Latest Updates

JAMANI JAMANI DUNIA INAELEKEA WAPI? ONA MAAJABU HAYA MSANII AZIKWA KAMA MBWA HUKO RORYA.


NI siku nyingine tena tunakutana hapa katika safu yetu ya kupeana dawa kuhusu mambo ya uhusiano na mapenzi. Sina shaka mtakuwa wazima wa afya njema kama nilivyo mimi. Karibuni uwanjani tupeane darasa. Leo nitazungumza juu ya jambo muhimu sana, uhusiano wa penzi la dhati na kukutana faragha. Kwa bahati mbaya, wengi wanaamini kwamba kukutana kimwili ndiyo kuoneshana mapenzi ya dhati, jambo ambalo si kweli hata kidogo.

Hebu tupeane changamoto kidogo, unafikiri mapenzi ni nini hasa? Kila mmoja anaweza kuwa na maana yake, lakini kimsingi mapenzi hayana maana ya moja kwa moja! Kwa ujumla mapenzi ni hisia zinazotoka moyoni mwa mmoja kwenda kwa mwingine, zikimaanisha upendo wa dhati.

Pendo hukamilika ikiwa wawili hao kwa wakati mmoja wakahisi hisia hizo, ingawa wakati mwingine mmoja ndiyo huwa wa kwanza kuanza kupata hisia hizo. Tafsiri hii nimewahi kuitaja mara kadhaa katika makala zangu, kama wewe ni mdau wa kona hii utakuwa unakumbuka, kama ndiyo kwanza unasoma hapa, basi si vibaya maana utakuwa umeingiza kitu kichwani mwako.

Wakati mwingine inawezekana mkajikuta mmependana tangu siku ya kwanza tu mlipokutana, lakini wengine huchukua muda mrefu kidogo kabla hisia hizo hazijachukua nafasi. Lakini wengine hufikiria mapenzi ni ngono au ngono ni sehemu ya mapenzi. Hawa nitapingana nao kwa nguvu zangu zote.

LAZIMA KUKUTANA FARAGHA?
Hakuna ulazima, wala faragha si kiashirio cha penzi la dhati. Mapenzi ni kitu kingine na ngono ni kitu kingine. Kimsingi ngono huja baada ya tamaa kuingia kati ya hao wawili wanaopendana.

Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa, ukawa na tamaa ya kufanya ngono na mtu hata kama huna mapenzi katika moyo wako. Kimsingi suala la kufanya ngono siyo kithibitisho cha kuonesha mapenzi ya dhati.
Baadhi ya walio katika uhusiano, hudanganywa na kipengele hiki. Utakuta msichana anaambiwa na boyfriend wake kwamba ili aoneshe kuwa anampenda basi lazima akubali kufanya naye ngono.

Hata hivyo, baada ya kumaliza kufanya hivyo, kuna uwezekano mkubwa wa penzi hilo kuyeyuka! Ni kweli ni rahisi kuachwa kwenye mataa hasa kama mhusika alikuwa ameshikwa na tamaa badala ya penzi la kweli.

MUDA GANI NI SAHIHI?
Kimsingi suala la kufanya mapenzi halina kanuni, hakuna muda maalum wa kuanza kufanya mapenzi na mpenzi wako mpya. Ngono ni hisia tu, tena basi huwa bora zaidi kama hisia hizo zikaja kwa wakati mmoja kati yako na huyo unayempenda.

Wataalamu wa Saikolojia ya Mapenzi, wanashauri wapenzi wasishiriki tendo hilo mpaka pale watapokuwa wamefahamiana kiasi cha kutosha juu ya tabia zao na historia zilizopita na husisitiza kitendo hicho kifanyike baada ya wapenzi husika kufunga pingu za maisha. Pamoja na hayo, suala la ngono halikwepeki ikiwa mtaruhusu kukutana sehemu tulivu mkiwa wawili.

Jambo la msingi ni kutulia na kujipanga, msifanye ngono kama sehemu ya mapenzi. Tambua kuwa ngono ni kitu kingine na mapenzi ni kitu kingine. Hata kama mtakuwa mmeamua kushiriki kitendo hicho, mfahamu kuwa mnastarehesha nafsi zenu tu na siyo kuoneshana mapenzi ya dhati.

TATIZO LIPO WAPI?
Tafiti mbalimbali za wataalamu wa mambo ya uhusiano, zinaonesha kuwa wengi walio katika uhusiano huwa hawawezi kuvumilia kuendelea kuwepo katika uhusiano bila kufanya mapenzi. Hata hivyo, tafiti hizo za uhakika zinaeleza kuwa baada ya wapenzi kufanya ngono, ile hamu ya kuendelea kuwa pamoja hupungua!

Hiyo husababishwa na dharau za kimaumbile na kujihakikishia kuwa hakuna kitu asichokijua kwa patina wake. Wengi hulia baada ya kujikuta wakiingia katika mkumbo huu. Hebu jiulize, kama anakupenda, kwanini anang’ang’ania kufanya mapenzi na wewe haraka?

Wewe ni wake na huenda mna ndoto za kuishi pamoja siku moja, kwa nini asivumilie mpaka wakati huo? Akitaka anaweza kuvumilia na kufaidi mambo hayo mkiwa katika ndoa.

FAHAMU MBADALA WAKE
Yapo mambo mengi  ya kufanya badala ya ngono, huna sababu ya kutoa kipaumbele kwa ngono wakati kuna vitu vingine vingi unavyoweza kufanya na kuyafanya mapenzi yenu yakaendelea kudumu kila siku.
Mnaweza kukaa sehemu nzuri yenye utulivu kwa ajili kupanga maisha yenu ya baadaye. Epukeni sehemu zenye vificho, ambazo zinaweza kuwapa vishawishi vya kufanya mapenzi. Lakini pia kutoka pamoja mitoko maalum hususan wikiendi hunogesha zaidi penzi.

Hata hivyo, kutumiana zawadi ni njia nyingine ambayo inaweza kunogesha penzi lenu na kuweka mambo ya ngono pembeni. Amini usiamini rafiki yangu, suala la faragha si muhimu sana katika uhusiano hasa mchanga. Mkifikia uamuzi huu ni lazima wote wawili mjadiliane na kufikia muafaka kabla ya kukimbilia, mwishowe uingie kwenye majuto.

0 Response to "JAMANI JAMANI DUNIA INAELEKEA WAPI? ONA MAAJABU HAYA MSANII AZIKWA KAMA MBWA HUKO RORYA. "

Post a Comment