1: Kufanya mambo fake.
Kuna wanawake hujiwekea nakshi kibao na vikolombwezo vya asili, lengo lake likiwa kuonekana tofauti mbele ya mwenzi wake siku ya kwanza. Hilo ni tatizo, kwani mnapozoeana, hutafanya hayo. Atakushusha thamani.
Simama wewe kama wewe, usijivalishe uhusika ambao hauna. Kuna wale wataalamu wa kujiunga ndimu ili kupunguza njia ionekane finyu. Sawa, utaweza kumfanya akuone hivyo, je, utafanya hivyo siku zote? Usisahau kwamba udogo wa barabara siyo tija. Hiyo uliyonayo itunze vizuri. Usafi ni muhimu sana.
Ni ukweli kwamba wanaume huwapenda wanawake wanaofurahia tendo lakini kufeki ni tatizo kubwa. Wapo mabingwa wa kupiga yowe au kutoa miguno inayoashiria raha hata kama wameguswa sehemu ambayo haiwasisimui.
Elewa kwamba kwa vile mwanaume hufurahia zaidi mwanamke anayefurahia tendo, pale atakapokugusa nawe ukasisimka au kutoa sauti zenye ishara fulani ya raha, hapo unakuwa umempa mrejesho kwamba alipopagusa ndipo anapotakiwa kugusa.
Huo mrejesho, utamfanya awe anatilia mkazo eneo ambalo lilikufanya utoe yowe. Sasa basi, kama ulifeki, utamsababishia aendelee kuwekeza maarifa yake kwenye sehemu ambayo siyo hasa inayokupa hamasa. Gharama za kufeki ni kubwa sana.
Kwa maana hiyo, siku ya kwanza kukutana na mwenzi wako, hakikisha unaonesha hisia za kweli. Kama sehemu haina mguso wowote kwako, hata akigusa mara ngapi, wewe jitulize kama maji mtungini. Akikupatia nawe ukapatikana, mpe mrejesho (sisimka) hapo utakuwa umemsaidia sana na mmejisaidia wote.
Kuna kufeki mpaka mshindo. Hajakufikisha kileleni wewe unamdanganya umefika. Matokeo yake, siku nyingine mkikutana, atakukuruka kwa uwezo uleule akiamini atakufikisha. Akikuuliza tena, utamjibu umefika. Unazidi kujiumiza.
Haya ni mapenzi ya kileo, mwanamke unatakiwa kuwa imara kutetea kile ambacho kinaweza kukufanya ufurahi. Mpenzi ni wako, usimwonee aibu na kumwongopea, mweleze ukweli wa hisia zako. Ikibidi mtumikishe hasa mpaka akupeleke unapopataka.
Kuwa huru, unaogopa nini nanyi mpo wawili tu? Mweleze waziwazi, msomeshe kuhusu maeneo yako ambayo unayajua kikamilifu kwamba yakifanyiwa utalii wa nguvu, utafika kwenye kilele cha raha. Usiache raha zipite juu, ruhusu ziingie ndani. Ruhusu mdomo wako utamke ukweli kwa mwenzi wako.
Kama kweli unampenda na unahitaji kudumu naye, lazima utamwambia ukweli. Usipomwambia unakuwa unajiweka njia panda. Ataendelea kukutendea chini ya kiwango, nawe utamuona hana jipya. Utamchoka, utachoshwa, mwisho utamdharau kabisa.
Uvivu wako wa kusema, aibu yako ya kutomweleza ukweli, vitakugharimu kwa sababu pengine unaweza kumuona hafai na ukaanzisha uhusiano mwingine na mtu ambaye utadhani atakupatia, kumbe huyo ndiye akawa hovyo kabisa.
Unaweza kuachana na mtu anayefaa sana, anayeweza kukupatia lakini hukujua jinsi ya kumtumia. Ulimdanganya hisia zako. Tuache porojo za mitaani, mwanaume hana uwezo wa kusoma kile kilichomo ndani ya fikra zako.
Wapo ambao baada ya kuchoshwa, huwatangazia marafiki au kuomba ushauri kwangu na kwa wataalmu wengine wa masuala ya uhusiano, wakilalamika kuwa wapenzi wao hawawafikishi. Unakuta huyo mlalamikaji, hajawahi kuzungumza kinagaubaga na mwenzie. Kosa kubwa!
Mwili ni wako, maeneo murua ndani yako unayajua mwenyewe. Mshirikishe mwenzio ili kuufanya muunganiko wenu uwe mzuri. Siku zote kemea udanganyifu, simamia kilicho sahihi. Kuna faida yingi zitafuata kwako kama tu utaacha kufeki.
0 Response to "Soma hapa makosa 10 ambayo wanawake wengi huyafanya wakiwa faragha sehemu ya pili "
Post a Comment